Misaada yawasili kisiwani Vanuatu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Malori yakibeba misaada.

Msaada wa dharura umeanza kuwasilishwa katika visiwa vilivyoathiriwa vibaya na kimbunga Pam nchini Vanuatu wiki iliyopita.

Makundi ya kutoa misaada yaliwasili katika mojawapo ya visiwa vikuu, Tannaa, kwa mara ya kwanza hapo jana.

Joe Lowry ambaye ni mkaguzi wa shirika la umoja wa mataifa la uhamiaji amesema kuwa kisiwa hicho kitahitaji msaada mkubwa na usaidizi katika wiki zijazo