Ubaguzi wa rangi upo Uingereza ?

Image caption Trevor Phillips

Swala la ubaguzi wa rangi limezua mjadala mkali miongoni mwa raiya wa Uingereza.

Asilimia kubwa ya raiya wa Uingereza wanasema wanazidi kushindwa kuzungumzia swala la kuwepo kwa raiya weusi na wale wasio wenye asili ya Uingereza.

Katika miaka ya hivi punde raiya wengi wa Uingereza wanasema kuwa wanazidi kubanwa na kuzomewa pindi wanapozungumzia swala hilo la ubaguzi wa rangi.

Katika ripoti moja iliyoandaliwa majuzi na ambayo itapeperushwa leo raiya wengi wa Uingereza wanasema hawawezi kuzungumzia kwa uwaziswala hilo bila ya kuzomewa kwa kuwa wabaguzi wa rangi.

Aliyekuwa mratibu mkuu wa halmashauri inayozingatia usawa Britain ,bwana Trevor Phillips,ametibua kidonda hicho cha ubaguzi dhidi ya watu wasiowenye asili ya kiingereza.

Mojawepo ikiwa kampeini ya kushinikiza usawa wa watu wenye asili ya Afrika na bara Asia.

Phillips alizunguka kote nchini Uingereza akikutana na jamii za watu waliodhulumiwa kwa misingi ya rangi yao na asili yao.

Mwenyewe akiwa mwenye asili ya visiwa vya Carribean ,alisema kuwa wengi wa watu ambao awali walidhaniwa kuwa wamedhulumiwa ,walikuwa wenyewe ndio wanaotoa misimamo mikali.

Na japo alifahamu fika kilichokuwa kikitendeka, Phillips alishindwa kuwaeleza maafisa wa usalama kilichokuwa kikitokota katika jamii ya Uingereza.

Mwaka wa 2005

Tukio la kigaidi la mwaka wa 2005 mjini London Uingereza kiliibua taharuki miongoni mwa maafisa wa usalama huku likiwaacha familia 52 zikiomboleza vifo vya wapendwa wao.

Phillips sasa anajuta kwanini hakusema kilichoibuka katika utafiti wake.

Haki miliki ya picha
Image caption Mijadala inayohusu ubaguzi wa rangi inafaa kufanywa kote Uingereza

UKIP

Chama cha upinzania cha UKIP sasa kimeweka uhamiaji kama mojawepo ya nguzo za sera zake.

UKIP inasema kuwa endapo watapigiwa kura watakatiza idadi kubwa ya wahamiaji wanaotaka kuingia Uingereza.

Katika ripoti hiyo itakayopeperushwa leo katika runinga nchini Uingereza,yamkini vyombo vya habari haswa watangazi wa Runing wanahofia sana kutamka maneno yanayoweza kuibua kashfa ya kuwa wanapendelea mtu

mwenye rangi nyeupe na kuwabagua watu weusi na watu wanaotokea uarabuni na Asia.

Kwa mujibu wa bwana Phillips hofu hiyo imeibua maswala mawili makubwa

Hakuna anayetaka kujadili usawa wa rangi

Watu wenye asilia ya Uingereza (Wazungu) ambao sasa wanaona kuwa hali halisia ya uhamiaji imeanza kubadilika kwa kiwango kikubwa ilhali hawana wa kumkimbilia kuzuia uhamiaji zaidi.

Wenyeji hao sasa wanawafokea wanasiasa ambao hawashughulikii hilo swala kuu la uhamiaji na usawa wa nafasi za ajira.

Hiyo ndiyo sababu kuu ya kushamiri kwa chama cha United Kingdom Independence Party (UKIP), ambacho kimesema njia moja ya kupunguza uhamiaji ni kwa uingereza kujiondoa kutoka kwa muungano wa ulaya.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiongozi wa chama cha UKIP Farage

Kulingana na UKIP Waingereza wazungu wameshindwa kujadili nafasi finyu za kazi kwa vijana wao huku wakishuhudia wenyeji waliohamia huko wakichukua uraiya wa Uingereza na kazi zao pia.

Usawa wa Kijamii

Majuzi vijana wenye asili ya Kisomali walipatikana na hatia ya kuhusishwa na ngono ya watoto wachanga.

Kule Rotherham, magenge ya jamii ya watu kutoka Pakistani pia walishikwa na kosa sawa na hilo.

Ajabu ni kuwa yamkini maafisa wa polisi waliokuwa wakifanya uchunguzi kuhusiana na kesi hizo inadaia waliogopa kutambua na kuwachukulia hatua watuhumiwa kwa hofu ya kuonekana kuwa wanawabagua watu kwa misingi ya asili yao.

Vilevile kuna lile tukio la mateso ya msichana mwenye umri wa miaka 8 Victoria Climbie ambaye ilidaiwa aliteswa na shangaziye wote wenye asili ya Ivory Coast.

Mtangazaji wa shirika la BBC la Top Gear Jeremy Clarkson alifutwa kazi kwa kumshambulia produsa wa kipindi hicho maarufu duniani .

Hata hivyo kabla ya hapo Jeremy alisifiwa kwa ''kuropokwa'' maneno ambayo yalikisiwa kuwa ya kejeli kwa Wahindi na hata kusema ''magari mabaya ni sawa na kustarehe kingono na mwanamke Mhabeshi''

Jeremy Clarkson

Image caption je maswala ya waafrika nchini Uingereza yatajadiliwa vipi ?

Na si yeye tu aliyeibua nipe nikupe kutoka kwa wasikilizaji, kuna mwandishi mwengine wa Idhaa ya dunia ya BBC Benedict Cumberbatch

- ambaye alisema kuwa kunahaja ya kuwepo kwa wasani weusi kwenye filamu za Uingereza.

Hata hivyo alikashiwa sana kwa kuwataja watu wenye asili ya kiafrika kuwa ''watu wenye rangi''

na hilo liliibua mjadala mkali ikisemekana kuwa ilikuwa na maneno ya kibaguzi.

Swali ibuka ni je maswala ya waafrika nchini Uingereza yatajadiliwa vipi ?

Katika miaka ya 70 watu weusi walitajwa kuwa watu wenye rangi.

Watafiti wengi sasa wanasema kuwa swala la ubaguzi wa rangi nchini Britain, wanasema kuwa lazima mjadala wa kitaifa kuhusiana na ubaguzi wa rangi ufanywe wazi wazi ilikuibua mtagusano upya na kuzuia chuki baina ya watu wenye rangi na wazungu.