Kim Kardashian aonywa ngono za kila mara

Image caption Mwanamke mwenye mvuto duniani, Kim Kardashian

Kila wakati inadhaniwa kuwa ni dhana tu juu ya kile kinachozungumzwa juu ya Kim Kardashian ,ingawa ilikuwa ni uvumi lakini sasa imethibitika.

“Kim Kardashian amekuwa akizungumzia sana suala la majaribio yake ya kutafuta mtoto mpya ,ingawa mpaka sasa bado hajabeba ujauzito,na sasa ameamua kupumzika katika majaribio yake ya kutafuta mtoto .Kim ambaye ana umri wa miaka thelathini na minne ana kiu kubwa ya kuiongeza familia yake iwe kubwa,lakini baada ya majaribio yake kushindwa amekubali kwamba si kazi rahisi kupata ujauzito wa pili.

Na hii ni baada ya kukutana na wataalamu kadhaa wa masuala ya wanawake ,na akawathibitishia huwa anafanya ngono mara mia tano kwa siku,wakamtaka apumzike kwa muda na kumweleza kuwa mambo hayaendi hivyo,ulimwengu unatambua kuwa mwanamke huyo ana mvuto wa kipekee hasa katika masuala ya ngono na ana mahaba mazito kwa mumewe Kanye West.

Lakini swali la kujiuliza, katika hali ya kawaida binaadamu ana uwezo wa kufanya ngono mara mia tano kwa siku? Hili haliingii akilini inaonekana kama ni habari ya kupikwa tu na Kim hatumii via vyake vya uzazi kwa kiwango cha hali ya juu kama inavyodaiwa.

Image caption Kwa raha zake

Haijalishi Kim Kardashian ni maarufu ama si maarufu kiasi cha habari zake kuandikwa kwa kiwango kikubwa ,lakini Kim alinukuliwa akisema kuwa mtoto wao wa kike North West amepewa nyumba yao yenye thamani ya dola za kimarekani milioni ishirini iliyoko Calabasas, California.

Ndani ya jumba hilo ,mtoto huyo ametengewa chumba cha michezo ambacho anakipenda mno,na inaelezwa kuwa mtoto huyo anapenda kuwa na sehemu yake, yenye nafasi yake.

Kim aliwaambia E! Online kwamba yeye pamoja na Kanye wanalifanyia matengenezo makubwa jumba lao kwa uangalifu mkubwa,ili iwe na muonekano mpya.Na anaeleza hisia zake kwamba kuwa katika jumba hilo ni uhuru mkubwa tofauti na alivyozoea kuishi na mamake katika nyumba yenye chumba kimoja .

Hivi karibuni Kim Kardashian alishangaza ulimwengu baada ya kuubadili muonekano wake kwa kuziweka nywele zake rangi ya gold wataalamu wa masuala ya saluni wenyewe wanaita blonde. Na inasemekana mtaalamu wa vipodozi Joyce Bonellindiye aliyemvutia na kuyafanya maamuzi hayo ya kuubadili muonekano wake. Wengine wanadhani anamuiga Madonna alipokuwa katika umri mdogo.haijalishi watu wanafikiria nini juu ya Kim,mwanamke huyo amekuwa gumzo na mvuto wa kipekee ulimwenguni na kufuatiliwa kila uchao na mamilioni ya watu kwa chochote afanyacho ,iwe wanapenda ama hawapendi.