Obama ampongeza Netanyahu kwa ushindi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Barack Obama wa Marekani

Rais Obama amemtumia salaam za pongezi waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kutokana na ushindi uliokipata chama chake katika uchaguzi uliofanyika Jumanne.

Lakini Bwana Obama ameelezea dhamira yake ya kuupatia ufumbuzi mgogoro kati ya Israel na Wapalestina kuwa ni kuunda taifa la Palestina.

Awali Ikulu ya Marekani ilielezea wasiwasi kuhusu ahadi ya Bwana Netanyahu wakati wa kampeni za uchaguzi kwamba asingeruhusu kuundwa kwa taifa la Palestina.

Waziri mkuu wa Israel tangu wakati huo amelegeza msimamo wake, akisema atakubali suluhisho la kuwepo mataifa mawili jirani endapo usalama katika eneo la Mashariki ya Kati utaimarishwa.