Rais wa Tunisia atangaza vita ya ugaidi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia

Rais Beji Caid Essebsi amesema kuwa nchi yake ipo katika vita dhidi ya ugaidi,kufuatia kuuawa kwa watalii 17 na raia wawili wa taifa hilo katika shambulio lililofanyika katika eneo maarufu la makumbusho.

Amesema nchi yake itakabiliana na watu hao waliohusika na mashambulizi hayo ya kinyama bila huruma.Kati ya raia hao wa kigeni waliouawa wanatoka mataifa ya Japan,na Italia.Watalii kutoka mataifa ya Colombia, Australia, Hispania,Ufaransa na Poland waliuawa pia.

Hata hivyo watalii hao walikuwa wakijiandaa kutembelea makumbusho ya Bardo karibu na eneo la bunge la nchi hiyo.

Watu hao waliokuwa wamejihami kwa silaha baada ya kufanya mauaji hayo walichukua mateka ndani ya jumba hilo la makumbushokabla ya wawili kati yao kuuawa,huku zaidi ya watu 40 wakijeruhiwa.