Tunisia yatangaza vita dhidi ya ugaidi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Caib Essebsi wa Tunisia

Rais wa Tunisia, Beji Caib Essebsi, amesema nchi yake imo vitani na ugaidi baada ya wanaume waliojihami kwa bunduki kuwaua watalii wa kigeni wapatao 17 na raia wawili katika shambulio katika makavazi mjini Tunis.

Kiongozi huyo amesema nchi yake itakabiliana pasi kuyasamehe na alichokitaja kama makundi madogo ya kishetani.

Washambuliaji hao waliwapiga risasi wageni kutoka Japan, Colombia, Australia, Italia na Uhispania kabla ya kuuawa na maafisa wa usalama.

Rais Beji Caid Essebsi amesema Tunisia ililazimika kupambana na magaidi waliokuwa wanahatarisha usalama wa nchi.