Sheria ya ajira kuhusu raia wa kigeni nchini tanzania yapitishwa
Huwezi kusikiliza tena

Sheria ya ajira za wageni TZ yapitishwa

Bunge la Tanzania limepitisha mswada wa sheria ya udhibiti wa ajira za wageni wa mwaka 2014, ambapo pamoja na mambo mengine unaainisha vipengele muhimu vya ajira kwa wageni na wazawa.

Hata hivyo, bunge hilo limeitaka serikali kupitia taarifa za waomba ajira wa kigeni ili kubaini uwezo wao katika ajira wanazoomba na mienendo yao kijamii.

Mwandishi wetu Leonard Mubali ana taarifa zaidi.