Je umetoboa sehemu za siri?soma hapa.

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Je umetoboa sehemu za siri? utashtakiwa Uingereza .

Wanawake wote walioamua kupamba sehemu zao za siri kwa kuzitoboa wanachukuliwa kuwa wamepitia ukatili wa kijinsia ama wamekeketwa kitengo cha afya kimetanabahisha hayo.

Hata kama mtu huyo amefikia umri wa utu uzima na ameyafanya hayo kwa ridhaa yake,bado atahesabika kuwa alipitia ukatili wenye madhara kwa afya yake,na inapaswa kuchukua tahadhari kubwa kuweka kumbu kumbu za watu walio toboa sehemu zao za siri.

Lakini kujichora mwilini maarufu kama Tattoo ama kutoboa sehemu za siri ama mwilini,kumepingwa na taasisi ya utoboaji na uchoraji tattoo mwilini kwamba hakuna uhusiano wowote na ukeketaji.

Na kueleza kuwa vitu hivyo viwili havichangamani kulinganisha na kutoboa sehemu za mwili wa mwanadamu,na taasisi hiyo wanachukulia suala la kutoboa mwili kama jambo la kaiwada na la ridhaa anasema msemaji wa taasisi hiyo Marcus Henderson.

Zaidi ya matukio ya ukeketaji yapatayo mia mbili yalichunguzwa na polisi wa kimataifa miaka mitano iliyopita,na inashauriwa kama kuna mtu mmoja ana mashaka na suala ya ukeketaji wataarifu polisi.

Watoboaji makini huwa hawataki kuumiza wateja wao na huwa hawataki kuonesha tundu za kazi zao na hawako tayari kumtoboa mtu aliye chini ya umri wa miaka kumi na nane,anaeleza Mr Henderson.

Image caption Mtoboaji maarufu amesema kwamba wateja wengi wanataka kutobolewa sehemu zao za siri

Mtoboaji maarufu kutoka mjini London ambaye ametaka ahifadhiwe jina lake, amesema kwamba wateja walio wengi huwa wanataka kutobolewa sehemu zao za siri zisilingane na ukeketaji.

Sihusiki na ukeketaji,nadhani utoboaji ni zaidi ya pambo mwilini ama uvumbuzi mpya wa kihisia zaidi.

Mtoboaji huyu anadai kwamba huwa anaitekeleza kazi yake kwa ufanisi mkubwa,kwanza huangalia picha kwa umakini mkubwa kabla hajamtoboa mtu, na kamwe hawezi kumtoboa mtu aliye na umri wa chini ya miaka kumi na nane.

Na wateja wake walio wengi ni wanawake na hutoboa sehemu ya siri hasa kwenye pezi la sehemu ya kati ya maungo ya mwanamke.

Ingawa mtoboaji huyu mashuhuri mwanzoni alikuwa hakubali kutoboa sehemu za siri za wanawake,na hii ni kutokana na maungo hao yalivyo na hatari inayowakabili kupitia utaratibu huo.

Naye msemaji kutoka kitengo cha afya ambaye ni mwanamke anasema kwamba,kuna changamoto kwa baadhi ya maeneo wanawake watu wazima hutobolewa sehemu zao za siri kilazima na maeneo mengine wasichana hulazimishwa kutobolewa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanawake waliotoboa sehemu zao za siri watachukuliwa kuwa wamepitia ukatili ama wamekeketwa

Idadi ya wanawake waliokeketwa nchini Uingereza inatajwa kufikia laki moja na elfu sabini,na zaidi ya wanawake na wasichana elfu mbili na mia sita wamehudumiwa na kitabibu tangu September na kati ya hao ,mia nne tisini na tisa walitambuliwa January mwaka huu pekee.

Nayo serikali ya Uingereza imesema kwamba haina mpango wa kuifanyia marekebisho sheria ya mwaka 2003 kuingiza suala la kufanya upasuaji kwa masuala ya urembo kwenye sehemu za siri.

Kamati teule ya wabunge katika taarifa yake imesema kwamba sheria hiyo haina budi kubadilishwa ili kuweka wazi juu ya taratibu hizo kuwa ni kinyume cha sheria na zaidi ni kosa la jinai kama zitafanywa kwa msichana wa chini ya miaka kumi na nane isipokuwa kwa sababu ya afya ya akili au kimwili.