Ugaidi:Kamanda wa polisi atimuliwa Tunisia

Image caption Waziri Mkuu wa Tunisia, Habib Essid, amewaachisha kazi makamanda wa polisi.

Waziri Mkuu wa Tunisia, Habib Essid, amewaachisha kazi makamanda wa polisi.

Hatua hii imechukuliwa mashambulizi katika jumba la ukumbusho katika mji mkuu wa Tunis ambapo zaidi ya watu 20 waliuawa - wengi wao wakiwa watalii.

Mara tu baada ya mashambulizi kwenye jengo hilo la ukumbusho la kifahari la Tunis, habari zilisambaa kuwa kulitokea etepetevu mkubwa wa walinda usalama katika eneo la jumba hilo la Bardo lililoko katikati mwa Tunis.

Uchunguzi wa Serikali unaelekea kuthibitisha madai hayo.

Kutokana na hayo maafisa wakuu sita wa polisi wameachishwa kazi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maafisa sita wakuu wanalaumiwa kwa etepetevu uliosababisha shambulizi hilo.

Na huku raia wa Tunisia wanapoendelea kuomboleza yaliyowapata kufuatia shambulio katika jengo hilo la ukumbusho, habari zingine zimetokea kuhusu mauaji mengine.

Mwanajeshi mmoja aliuawa wakati gari laki lilipokanyaga bomu lililokuwa limetegwa ardhini katika maeneo ya milima,

eneo la Magharibi linalotambuliwa kuwa na wapiganaji walio na uhusiano wa karibu na kundi la Al Qaida.