Marekani kuimarisha uhusiano na Iran

Haki miliki ya picha v
Image caption Rais Barack Obama wa Marekani

Rais Obama ametoa ujumbe katika kanda ya video kwa viongozi na raia wa Iran akisema kwamba hapajakuwa na wakati muafaka zaidi katika miongo kadha iliyopita kwa Marekani na Iran kutafuta uhusiano mpya.

Katika ujumbe wa kusherehekea mwaka mpya wa Iran, amesema mataifa hayo mawili yana fursa ya kihistoria ambayo haipaswi kupotea.

Amesema mazungumzo kuhusu mpango wa nuklia wa Iran yamepiga hatua lakini ameonya kuwa kuna watu wanaopinga mazungumzo juu ya mpango huo kwa nchi zote mbili yaani Marekani na Iran.

Bwana Obama amesema Wa-Iran watapata taabu zaidi kwa kutengwa kimataifa iwapo viongozi wao watachukua uamuzi mbaya.