Maiti 70 zapatikana zimetupwa Nigeria

Haki miliki ya picha AFP PHOTO NIGERIAN ARMY
Image caption Wanajeshi wa Nigeria

Takriban maiti 70 zimepatikana zimetupwa nje ya mji wa Damasak kaskazini mashariki mwa Nigeria baada ya mji huo kutwaliwa kutoka kwa kundi la Boko Haram.

Watu hao wanaonekana kuuawa siku kadha zilizopita ambapo baadhi ya maiti zilikuwa zimekatwa shingo.

Mji wa Damasak ulio karibu na mpaka na Niger ulidhibitiwa na wanamgambo wa Boko Haram mwezi Novemba mwaka uliopita lakini ukatwaliwa na wanajeshi kutoka nchini Niger na Chad siku ya Jumamosi.

Boko Haram wamewaua maelfu ya watu kwenye kampeni yake ya kutaka kubuni taifa la kiislamu kaskazini mwa Nigeria.