IS yataka Wanajeshi 100 wa US wauwawe

Haki miliki ya picha AP
Image caption Jeshi la Marekani linasema kuwa limeanza kuwajulisha wanajeshi 100 wa Marekani waliotajwa katika mtandao wa IS unaotaka wauawe

Jeshi la Marekani linasema kuwa linawajulisha karibia wanajeshi 100 waliotajwa kwenye orodha ya mtandao ulionzishwa na Islamic State unaotaka wauawe.

Kitengo cha kudukua mitandao cha Islamic State kinawataka wale wanaolipendelea kundi hilo kuwaua wale walio kwenye orodha hiyo ambao Islamic State inawalaumu kwa kuendesha mashambulizi ya angani dhidi yake nchini Iraq na Syria.

Majina yao, picha na namba zao zimechapishwa kwenye mitandao.

Kitengo cha ujasusi cha jeshi la wanamaji la Marekani kinasema kuwa tishio hilo halijathibishwa rasmi .

Kitengo hicho kinawataka wanajeshi kuchukua tahadhari kuhusu ujumbe unaowahusu wanaoweka kwenye mitandao.