Ulimwengu waomboleza kifo cha Lee Yew

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Yew aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 91

Waziri mkuu mwanzilishi wa Singapore, Lee Kuan Yew amefariki dunia.

Lee amefariki akiwa na umri wa miaka tisini na mmoja kutokana na ugonjwa wa mapafu.

Kwa miongo mitatu ya utawala wa Lee alifanikiwa kuipitisha nchi yake katika kipindi cha mpito na kuleta mabadiliko makubwa

ya kiuchumi hasa katika usafirishaji majini kwa kutumia rasilimali kidogo walizokuwa nazo na sasa kuwa kitovu kikubwa cha kibiashara cha kimataifa.

David Adelman ni balozi wa zamani wa Marekani nchini humo, ametuma salamu zake za rambi rambi.

Kifo cha Lee ni mwisho wa enzi zake.

mwisho wa mwanamume mwenye nguvu ya ushawishi aliyeingia madarakani katikati ya miaka ya sitini .

Lee alifanikiwa kuanzisha ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi yake na Marekani ambao umedumu hata leo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waombolezaji wakiweka mashada ya maua mbele ya hospitali aliyofia baba Lee Kuan Yew.

na unaweza kuvuka mipaka sio kwa singapore tu bali hata kwa watu wa Asia ya kusini Mashariki.

Viongozi mbalimbali duniani wanaendelea kutuma risala za rambirambi kwa Singapore, baada ya kifo cha Lee Kuan Yew hospitalini.

Yew aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 91 baada ya kuugua homa ya mapafu.

Nchini Uchina, wizara ya mashauri ya nchi za kigeni imemsifia na kumtaja Lee Kuan Yew, kama kiongozi wa kipekee wa bara Asia.

Marehemu Lee ambaye aliiletea mabadiliko makubwa taifa la Singapore na kuwa na mojawepo ya bandari maarufu zaidi Duniani huku uchumi wa nchi hiyo ukiimarika maradufu, atasalia katika kumbukumbu la taifa hilo.

Mwanawe ambaye ni waziri mkuu wa sasa nchini humo, Lee Hsien Loong, anasema kuwa Singapore haitawahi kuwa na mtu kama huyo tena.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Lee alifanikiwa kuanzisha ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi yake na Marekani

Katika risala zake za rambirambi, Rais Barrack Obama wa Marekani amemtaja kama gwiji wa historia.

Nchini Uchina, wizara ya mashauri ya nchi za kigeni imemsifia na kumtaja Lee Kuan Yew, kama kiongozi wa kipekee wa bara Asia.

Naye waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, anasema kuwa Bwana Lee alikuwa mmojawepo wa viongozi wakuu duniani.

Serikali ya Singapore imetangaza siku sita ya maombolezo, hadi atakapozikwa siku ya Jumapili.