Suge Knight aanguka mahakamani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Marion Suge Knight

Mahakama kuu imemuachilia kwa dhamana ya dola millioni 25 msanii wa muziki wa rap Suge Knight ,ambaye anatuhumiwa kwa kuwagonga wanaume wawili katika eneo la Campton nchini Marekani ,na kumuua mmoja.

Mda mfupi baada ya kusikizwa kwa kesi yake msanii huyo mwenye umri wa miaka 49 alianguka na kuzirai mahakamani ,ikiwa ni mara ya tatu kwa yeye kupelekwa hospitalini kufuatia kusikizwa kwa kesi yake.

Wakili wake alisema kuwa macho ya mteja wake yalianza kucheza cheza kabla ya kuanza kutokwa na jesho na mwishowe kuanguka huku akigonga kichwa chake katika meza na kupoteza fahamu.

Knight anatarajiwa kurudi mahakamani mwezi Aprili 13 ambayo ni siku ya kusikilizwa kwa kesi yake.

Katika kusikizwa kwa ombi la kutaka kuwachiliwa kwa dhamana, Suge Knight alishtumiwa kuwa muhalifu asiyetubu.