Marekani yawaondoa wanajeshi wake Yemen

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Marekani imewaondoa wanajeshi wake wote waliokuwa nchini Yemen

Wizara ya mashauri ya kigeni nchini Marekani imethibitisha kuwa wanajeshi wote wa Marekani waliokuwa wamebaki nchini Yemen ambao ni wanajeshi 100 maalum wameondolea nchini humo kufuatia kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa litaandaa kikao cha dharura leo jumapili kuzungumzia hali inayozidi kuwa mbaya nchini humo.

Mkutano huo ulipendekezwa na rais wa Yemen Abd Rabbuh Mansour Hadi ambaye mwezi uliopita aliukimbia mji mkuu Sanaa.

Kiongozi anataka waasi wa shia wa Houthi waondoke mjini huo mkuu.

Waasi wa Houthi nao wanapanga mikakati ya kuweza kukabiliana na wanajeshi watiifu kwa rais.