Ebola bado tishio

Haki miliki ya picha c
Image caption Mgonjwa wa Ebola akisaidiwa

Mashirika ya utoaji misaada yanaonya hali bado ni tete, mwaka mmoja tangu ugonjwa wa Ebola kulipuka magharibi mwa Afrika.

Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka- MSF, linasema kuwa mlipuko huo ambao uliwauwa zaidi ya watu elfu kumi.

Shirika limesema namna mashirika ya matibabu na watoaji misaada ya dharura, yalivyoendesha shughuli za kuwaokoa watu kuwa ni taratibu mno.