Mwandishi habari ashtakiwa Angola

Image caption Mwandishi mmoja wa habari mashuhuri ambaye pia ni mkereketwa wa haki za kibinadamu amefikishwa mahakamani nchini Angola kwa mada

Mwandishi mmoja wa habari mashuhuri ambaye pia ni mkereketwa wa haki za kibinadamu amefikishwa mahakamani nchini Angola kwa madai ya kuwaharibia watu majina.

Majenerali wa kijeshi saba walitoa madai hayo dhidi ya Raphael Marques, baada ya kuandika kitabu kilichowahusisha na mauaji,

mateso na unyakuzi wa ardhi katika maeneo yenye thamani nyingi yanayochimbuliwa almasi.

Mashtaka sawa na hayo yaliyowasilishwa nchini Ureno yalutupiliwa mbali na mahakma kutokana na ukosefu wa ushahidi.

Akipatikana na hatia, Rafael Marques, anakabiliwa na kifungo cha miaka tisa gerezani na faini ya Dola Milioni Moja Nukta mbili.

Anasema kuwa yeye haogopi kwa sababu ni kazi yake kuchunguza ufisadi na ukiukaji wa haki za kibinadamu.

Image caption Dos Santos amekuwa madarakani kwa kipindi kirefu

Tayari amedumu kwa muda gerezani - zaidi ya siku 40 katika seli ya kipekee baada ya kuandika kitabu cha ''The Lipstick of Dictatorship''

juu ya rais Jose Edwardo dos Santos, ambaye ametawala kwa zaidi ya miaka 35.

Nchini Angola watu hawaruhusiwi kutoa maoni ya kupinga Serikali.

Wakosoaji wa Serikali hunyamazishwa kwa kuhongwa, kufungwa au hata kuuawa.