Mabibi harusi wa zamani Zimbabwe waongea

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Raisi wa Zimbabwe Robert Mugabe

Mabibi harusi wa zamani wawili wameamua kuipeleka serikali ya Zimbabwe mahakamani katika harakati za kuvunja sheria kandamizi nchini humo na kutaka sheria inayoruhusu mabinti kuolewa wakingali wadogo iwe ni kinyume na katiba na si halali kwa kifupi iharamishwe.

Mabibi harusi hao Loveness Mudzuru na Ruvimbo Tsopodzi wamesema ndoa za utotoni ,ambazo ni ruksa nchini Zimbabwe,wansema ni sawa na ukatili wa kijinsia kwa watoto ambao huwanasa mabinti na kuishia katika janga la umasikini na madhila yasiyosemeka.

Nimekabiliana na changamoto zisizosemeka ,mume wangu alikuwa akinipiga sana.nilikuwa natamani kuendelea na masomo lakini yeye alikataa.nilikuwa na hali mbaya sana huu ni ushuhuda wa Tsopodzi, mama wa mtoto mmoja,mama huyu aliolewa akiwa na umri wa miaka kumi na mitano tu .

Na anaendelea kusema kwamba anataka kuchukua hatua hiyo ili kuleta tofauti,ameeleza hayo akiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare mapema wiki hii.Na hii yote ni katika harakati za kuzuia mabinti wadogo wanaoolewa katika umri mdogo.

Takwimu zilizochapishwa mwaka wa jana zinaonesha kwamba moja ya tatu ya wasicha walio na umri wa chini ya miaka kumi na nane huolewa , wakati wengine wapatao asilimia tano huolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka kumi na mitano.

Katika tamko lao kwa mahakama ya katiba, Tsopodzi na Mudzuru, ambao kwa sasa wana miaka 19 na mwingine ana miaka 20, wanasema kwamba sheria ya ndoa nchini Zimbabwe ni ya kibaguzi kwani inamtaka mtoto wa kike aolewe akiwa na umri wa miaka kumi na sita wakati mtoto wa kiume anatakiwa kuoa akishatimiza umri wa miaka kumi na nane, na ndoa za kimila hazijaainisha umri halisi wa kijana ama binti kuoa ama kuolewa.

Sheria ya ndoa ya mwaka 2013 inasema kwamba kila mtoto mwenye umri wa miaka kumi na mitatu,anayo haki ya kupata malezi ya wazazi,elimu na ulinzi kutoka kwao katika masula ya unyonyaji kingono na kiuchumi.

Sheria hii pia haijaweka wazi umri wa kuoa ama kuolewa lakini inasisitiza kwamba hakuna mtu yeyote atakayelazimishwa kuoa ama kuolewa kinyume na matakwa yao na kuonesha wazi kuwa raia wa Zimbabwe mwenye umri wa miaka kumi na nane anaweza kuwa na familia yake.

Umasikini ndio chanzo cha ndoa za utotoni nchini Zimbabwe na kuwasababisha kuolewa kabla ya umri wao wasichana walio wengi ,na hivyo kuwasababisha wazazi kupunguza mzigo wa familia katika masuala ya matunzo na kubakisha mama tu na baba.ulipwaji mahari nayo ni motisha inayowafanya wazazi kutowatendea haki watoto wao.

Baadhi ya familia nchini Zimbabwe zinatukuza ndoa za utotoni kwa mtazamo wa kuwalinda watoto wao wa kike na ngono kabla ya ndoa.

Mudzuru anatoa ushuhuda wake kwamba ndoa za utotoni ni chagamoto kubwa ,kwani mabinti hao walio katika umri mdogo watazaa watoto wakiwa katika familia masikini na hapo ndipo mzunguuko wa ndoa za utotoni unapoanza upya.

Mudzuru, aliolewa akiwa na umri wa miaka kumi na sita kwa sasa ana watoto wawili tena akiwa hajatimiza miaka kumi na nane ,anasema maisha yake yalikuwa sawa na jehanamu ya moto na aliishi maisha yake katika dhiki isiyosemeka.

Nasema maisha yake yalikuwa magumu sana, kulea watoto ilhali wewe mwenyewe ukiwa ni mtoto ni vigumu,na asema katika umri wake alipaswa kuwa anahudhuria masomo shuleni.

Naye mwanasheria wa mabinti hao ambao ni akina mama sasa hivi,alikuwa ni waziri wa zamani wa fedha nchini humo Tendai Biti, aliwasilisha changamoto hizo za kisheria mwezi January mwaka huu.

Beatrice Savadye,yeye ni mwanaharakati wa kupinga ndoa za utotoni nchini humo anayeongoza asasi isiyokuwa ya kiserikali,ijulikanayo kaka ROOTS ,asasi ambayo inawaunga mkono akina mama hao wawili anasema kesi hiyo imekuwa na mvuto wa kipekee nchini humo nan je ya nchi hiyo kwa ujumla wake.

Na anamashaka kama mahakama itatoa maamuzi yake lini ,lakini inalazimika kutoa maamuzi yake ndani ya miezi sita.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wazimbabwe

Ulimwenguni kwa ujumla wake wasichana milioni kumi na tano wanaolewa kila mwaka.katika jangwa la sahara peke yake asilimia arobaini ya wanawake huolewa wakiwa katika umri mdogo.