David Cameron: Awamu mbili zatosha!!

Haki miliki ya picha .
Image caption David Cameron

Waziri mkuu wa Uingereza, hataendelea tena na wadhfa wake huo, iwapo atarudi madarakani katika uchaguzi mkuu wa mwezi Mei.

David Cameron, ameiambia BBC kuwa, anadhani awamu ya tatu inaweza kuwa ni kipindi kirefu kwake kukaa madarakani na kiongozi mpya ni vizuri kuchaguliwa.

Chama kikuu cha upinzani cha Leba kimemshutumu Bwana Cameron kwa kuonyesha uzembe na kushinikiza muhula wa tatu, kwa chama chake cha Conservative, hata kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu ujao.