Ngome ya rais yashambuliwa Yemen

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waasi wa Houthi wateka mji wa Aden ambayo ni ngome kuu ya rais Mansour Hadi

Ndege za kivita nchini Yemen zimerusha makombora katika wilaya moja iliopo katika mji wa kusini wa Aden ambapo rais Abd Rabbuh Mansour Hadi anaishi.

Kuna ripoti za kutatanisha kuhusu aliko bwana Hadi ,ijapokuwa washauri wake wanasema kuwa yuko salama.

Waasi wa Houthi wakisaidiwa na vikosi vya aliyekuwa rais Ali Abdullah Saleh wanakaribia mji wa Aden baada ya kuiteka kambi moja ya kijeshi yapata umbali wa kilomita 40.

Waasi wa Houthi wametangaza zawadi kwa mtu yeyote atakayemkamata rais Mansour Hadi.

Waziri wake wa maswala ya kigeni ametoa wito kwa mataifa ya kiarabu kuingilia kati kijeshi.

Waasi wa Houthi waliuteka mji muhimu wenye uwanja wa ndege wa kijeshi kutoka kwa wanajeshi walio watiifu kwa rais wa Yemen Abdrabbuh Mansour Hadi huku wakiikaribia ngome yake ya Aden.

Wakaazi wa eneo hilo wanasema kuwa wapiganaji hao wanaoungwa mkono na vikosi vidogo waliuteka mji wa Al-Anad mapema siku ya jumatano baada ya mapigano makali.

Saa kadhaa baada ya kutekwa kwa kambi hiyo yapata kilomita 67 kazkazini mwa Aden.

Kuna ripoti kwamba rais Hadi alitoroka nyumbani kwake hadi eneo lisilojulikana.

Lakini washauri wa rais huyo walikana kwamba amnelitoroka taifa hilo.

Bwana Hadi alikimbilia usalama wake mjini Aden mwezi uliopita baada ya kutoroka Sanaa.

Waasi walichukuwa udhibiti wa mji mkuu mnamo mwezi januari ,na kumuweka rais huyo katika kifungo cha nyumbani huku wakitangaza kuwa baraza la viongozi watano litaongoza taifa hilo.