Kinasa sauti cha ndege chaharibika

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Milima ya Alps

Waziri wa maswala ya ndani nchini Ufaransa, Bernard Cazeneuve, amesema kuwa kifaa cha kunasa sauti kwenye ndege kilichopatikana hapo jana Jumanne baada ya kuanguka kwa ile ndege ya Ujerumani katika milima ya Alps kimeharibika.

Lakini Bwana Cazeneuve anasema kuwa kifaa hicho bado kitatoa taarifa kwa watalamu wanaojaribu kubaini kilicho sababisha kuanguka kwa ndege hiyo, ambayo iliwauwa abiria wote 150 na wahudumu waliokuwemo kwenye ndege hiyo.

Shughuli za utafutaji wa ndege hiyo zimerejelewa baada ya usiku kumalizika.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Milima ya Alps

Ndege za helikopta zinaonekana zikipaa katika maeneo hayo huku maafisa wa polisi wakiendelea kuchunguza mabaki ya ndege .

Maafisa wakuu wanaonya kuwa kupata mabaki ya miili ya abiria itachukua muda mrefu kutokana na hali mbaya ya anga katika eneo hilo.

Ndege hiyo ilikuwa ikitoka Barcelona na kuelekea mji wa Duesseldorf.

Kansela wa Ujerumani pamoja na Rais wa Uhispania na waziri wake mkuu, wanatarajiwa kuzuru eneo la ajali hiyo hii leo Jumatano.