Awaua wanawe na kuwaweka ndani ya Jokofu

Image caption Polisi waliogundua maiti hizo wakishika doria nje ya nyumba hiyo

Mwanamke mmoja amekamatwa na polisi kufuatia mauaji ya wanawe wawili waliopatikana wamefungikiwa ndani ya jokofu.

Maafisa wa polisi wanasema kuwa mwanamke huyo mama wa watoto wanne aliwatumbukiza wanawe wawili wenye umri wa miaka 11 na mwengine mwenye umri wa miaka 14 ndani ya jokofu baada ya kuwaua.

Aidha miili ya mvulana 11, na msichana 14, ilipatikana imewekwa kwenye karatasi za plastiki ilizisivunde.

Yamkini miili hiyo ilipatikana na maafisa wa idara ya mahakama waliokwenda nyumbani kwa mama huyo kwa nia ya kumfurusha baada ya kushindwa kugharamia kodi ya nyumba .

Walishtuka kupata miili ya watoto hao na mara moja wakawaarifu maafisa wa polisi katika jimbo hilo.

Wanawe wawili waliosalia walikuwa kwa jirani na walichukuliwa na kupewa usalama.

Uchunguzi na upasuaji wa maiti unatarajiwa kufanyika ilikubaina kiini haswa cha vifo vyao.

Afisa mkuu wa polisi katika jimbo hilo James Craig ametaja kitendo cha mwanamke huyo kuwa cha kuogofya mno.

Jirani ya mwanamke huyo Tori Childs, aliliambia shirika la habari la AP kuwa watoto hao wawili waliopatikana walikuwa wametoweka kwa takriban mwaka mzima .

Majirani wengine walisema kuwa mwanamke huyo alikuwa taabani haswa baada ya kushindwa kulipa kodi ya nyumba, na kuwa mama huyo mwenye umri wa

miaka 36 alikuwa kanakwamba anakabiliwa na upungufu fulani maishani mwake.