Marekani kushambulia IS mjini Tikrit

Image caption Rais wa Iraq Fouad Massoum

Rais wa Iraq Fouad Massoum ametoa ishara kwamba jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani huenda likatekeleza mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Islamic State mjini Tikrit.

Katika kipindi cha siku chache zilizopita, muungano huo ulianza kufanya uchunguzi katika mji huo wa Iraq.

Bwana Massoum ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba baada ya kukusanya ripoti za uchunguzi wa ndege,muungano huo utaanza oparesheni za kijeshi.

Hadi kufikia sasa ,Marekani imejiondoa katika jaribio la vikosi vya Kishia vya Iran kuuteka mji wa Tikrit.

Hatahivyo jaribio hilo limefeli huku mamia ya wapiganaji wa ISIS wakisalia katikati ya mji.

Rais wa Iraq hajasema iwapo serikali ilitaka mashambulizi ya angani ya Marekani katika mji wa Tikrit.