Raia wa Singapore wamuaga Lee Kuan Yew

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jeneza la aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza nchini Singapore Lee Kuan Yew

Maelfu ya watu wamepiga foleni nje ya majengo ya bunge nchini Singapore, ili kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa nchi hiyo Lee Kuan Yew.

Marehemu Lee Kuan Yew aliyefariki siku ya jumatatu akiwa na umri wa miaka 91 atazikwa siku ya jumapili.

Mashirika na kampuni nyingi ya kibiashara zimewapa wafanyikazi wao ruhusa ya kwenda kumuaga marehemu Lee kwa heshima na taadhima.