Mkurugenzi wa '50 Shades of Grey' ajiuzulu

Image caption Filamu ya Fifty Shades of Grey

Mkurugenzi wa filamu ya Fifty Shades of Grey ambayo imepigwa marufuku nchini Kenya Sam Taylor-Johnson hatoendeleza uelekezaji wa misururu miwili ya filamu hiyo.

Msanii huyo amesema kuwa anashukuru sana kwa kuchaguliwa kuendeleza utunzi wa kitabu cha EL james's 2011 ambacho kimeuza sana.

Baadaye aliwatakia mafanikio wale watakaomrithi ili kuendeleza misururu miwili iliosalia ya filamu ya Fifty Shades of Grey.

Filamu hiyo iliohusu mfanyibiashara anayeanzisha uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi imetenegeza karibia dola millioni 560 katika mauzo.

Uhusiano kati ya James Taylor na mtunzi wa filamu hiyo ulidaiwa kuzorota wakati wa utayarishaji wa filamu hiyo na kuzua madai kwamba msanii huyo ambaye pia ni mtayarishaji wa filamu hatarudi kuendeleza maudhui ya filamu hiyo.