Marekani yashambulia Tikrit nchini Iraq

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ndege za jeshi la marekani zimeshambulia mji wa Tikrit nchini Iraq

Ndege za kijeshi za Marekani zimeanza kutekeleza mashambulizi makali, katika maeneo yenye wanamgambo wa Islamic State, katika mji wa Tikrit uliotekwa na waasi hao.

Vifaru vya jeshi la Iraqi pia vimerejelea mashambulizi makali ya ardhini katika mji huo.

Kiongozi mmoja mkuu wa Marekani, anasema kwamba mashambulio ya angani kwa maeneo yanayolengwa, yanafuatia ruhusa kutoka kwa serikali ya Iraq.