UK kuwapa mafunzo ya kijeshi waasi Syria

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wanajeshi wa Uingereza

Uingereza imesema kuwa itatoa mafunzo ya kijeshi kwa waasi wa Syria wanaokabiliana na serikali ya rais Bashar Al Asaad,kwa mujibu wa katibu wa ulinzi nchini Uingereza Michael Fallon.

Karibia wakufunzi 75 pamoja na wafanyikazi wengine wa makao makuu watasaidia katika matumizi ya silaha ndogo ndogo,mbinu za kijeshi pamoja na zile za matibabu.

Mafunzo hayo yatafanyika nchini Uturuki ikiwa ni miongoni mwa mipango ya serikali ya Marekani.

Bwana Fallon amesema kuwa wapiganaji wa Islamic state wanaweza kushindwa na vikosi vya maeneo hayo katika ardhi za Syria na Iraq.

Amesema kuwa nchini Syria mashambulizi ya vikosi vya muungano yameharibu mipango ya IS pamoja na njia zao za kupata silaha