Je utanunua simu iliyotengezwa na Nyasi ?

Image caption Je utanunua simu iliyotengezwa na Nyasi ?

Watu wengi wamekuwa wakilalamikia teknolojia na ufundi wa simu nyingi za kisasa wengi wakiwaponda wabunifu kwa misingi ya kuwa

asilimia kubwa ya simu za mfumo wa 3G na zaidi zinatengezwa kwa plastiki.

Sasa basi,bwana mmoja mbunifu amekuja na jibu ya kutengeza simu kutokana na ''Nyasi'' .

Bwana Sean Miles amezindua simu itakayokuwa ya kipekee.

Simu hiyo ndiyo ya kwanza kuwahi kutengenezwa kwa asilimia 100% kutokana na bidhaa hai.

Gamba la juu la simu hiyo limeundwa kwa bidhaa inayotokana na nyasi maalum iliyochanganywa na kemikali fulani na kiungo (resin)

"mchanganyiko huu maalum unatoa sura kama vile (carbon) alisema Miles.

Mfumo huo unachanganywa na kumbwa kwa njia itakayoruhusu watengezaji wa simu kuumba gamba la simu inayotokana na nyasi.

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Simu nyingi za kisasa hazina ubunifu na zinaelekea kufanana

Bwana Miles alikuwa amepewa kandarasi na kampuni ya simu ya O2 kutafuta mbinu ya kutumia upya bidhaa ambazo zimekosa wateja ama zimezeeka.

Hata hivyo kitengo cha ubunifu kilitamaushwa na ubunifu wake na sasa kimeanza mikakati ya kutathmini uwezo wa kampuni hiyo kuunda kwa wingi magamba ya simu.

Kufikia sasa asilimia 25% ya simu nzee nchini uingereza zinarekebishwa na kutumiwa upya.