Mtandao wa kiislamu kukabiliana na IS

Image caption Mtandao wa kiislamu wa kukabiliana na uvumi wa islamic state wazinduliwa

Viongozi wa kiislamu kutoka matifa tofauti ya Ulaya wameanzisha jarida la mtandaoni katika juhudi za kukabiliana na itikadi kali za kidini zinazoendeshwa na wapiganaji wa Islamic State.

Jarida hilo la kidijitali kwa jina ''Haqiqah'' ama ''Ukweli'' limezinduliwa na mtandao wa Imam na unalenga kuwafunza vijana wadogo kuhusu ukweli wa makundi ya itikadi kali.

Imam hao wanasema kuwa wana wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa uvumi unaozushwa na makundi hayo katika mtandao,na kwamba jarida hilo jipya ndio njia pekee ya kukabiliana na uovu,na mawazo mabaya.