Sharapova atupwa nje michuano ya Miami

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Maria Sharapova mcheza tenisi nambari mbili duniani

Sharapova anayeshikilia nafasi ya pili kwa ubora duniani alikubali kichapo cha seti 7-6 (7-4) 6-3 kutoka kwa Daria Gavrilova anayeshikilia nafasi ya 97 kwa ubora wa mchezo huo duniani.

Katika mchezo mwingine Caroline Wozniacki, alimgaragaza Madison Brengle wa Marekani kwa seti 6-0 6-1.

Kwa upande wa wanaume Vasek Pospisil wa Canada alipata ushindi wa kishindo dhidi ya mpinzani wake Juan Martin Del Potro toka Ajentina kwa seti 6-4 7-6 (9-7)

Michezo mingine ya leo, mchezaji nambari 3 kwa ubora duniani Rafael Nadal atachuana na Nicolas Almagro, huku Andy Murray akionyeshana kazi na Donald Young wa Marekani.