Rubani alikuwa na matatizo ya kiakili

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ajali ya ndege

Viongozi wa mashtaka nchini Ujerumani wanasema kuwa wamepata ushahidi unaosema kwamba rubani wa ndege ya Ujerumani ilioanguka katika milima ya ALPS na kuwaua abiria 150 alikuwa amemficha mwajiri wake kuhusu ugonjwa anaougua.

Maafisa hao pia wamesema kuwa walipata kijikaratasi cha ugonjwa kilichokuwa kimekatwa ambacho kilimtaka rubani huyo kupumzika siku ya kuanguka kwa ndege hiyo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maafisa wa Polisi wa ujerumani

Hatahivyo hawakupata ujumbe wowote wa rubani huyo kutaka kujitoa uhai wake.

Vyombo vya habari nchini Ujerumani vimeripoti kwamba faili ya rubani Andreas Lubitz mwenye umri wa miaka 27 katika shirika la anga za juu imeonyesha kuwa Andreas alikuwa na matatizo ya akili na alitakiwa kufanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Andreas Lubitz

Ripoti nyengine ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa alilazimika kuchukua likizo ya miezi sita kutoka kwa mafunzo ya urubani kutokana na shinikizo la akili.