Mawaziri 4 wasimamishwa kazi Kenya

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewasimamisha kazi mawaziri wanne katika serikali yake kufuatia madai ya ufisadi yanayowakabili

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewasimamisha kazi kwa mda mawaziri wake wanne pamoja na maafisa wengine 12 wa ngazi ya juu katika serikali yake kufuatia madai ya ufisadi.

Waziri mwengine wa tano amejiondoa afisini akisubiri kuchunguzwa na madai hayo.

Maafisa hao walitajwa katika ripoti ya ufisadi mapema wiki hii na tume ya ufisadi nchini Kenya .

Kashfa hizo za ufisadi zinadaiwa kuzikabili wizara za Uchukuzi,Kawi,Kazi na kilimo.

Rais Kenyatta ameipa tume ya kukabiliana na ufisadi siku 60 kuchunguza madai hayo.