Saudia yawaondoa raia wake Yemen kusini

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mji wa kusini wa bandari ya Aden nchini Yemen

Vyombo vya habari nchini Saudi Arabia vinasema kuwa nchi hiyo imewahamisha raia wake na wanadiplomasia wa kigeni kutoka mji wa bandari ya Aden kusini mwa Yemen.

Jeshi la wanamaji la Saudi Arabia liliongoza oparesheni hiyo.

Kundoka kwa watu hao kunajiri wakati waasi wa Houthi wanazidi kuelekea mji wa Aden.

Saudi Arabia iliongoza mashambulizi ya siku tatu dhidi ya waasi hao wanaoungwa mkono na Iran lakini hayo yote yameshindwa kuwazuia kusonga mbele

Wakaazi wameeleza kuwepo kwa mashambulizi makubwa ya angani kwenye mji mkuu wa Yemen, Sanaa.