Ebola:Guinea yatangaza hali ya dharura

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Alpha Konde

Rais wa Guinea ametangaza hatua za dharura kwenye majimbo matano ya nchi hiyo katika mpango mpya wa kuangamiza ugonjwa wa ebola.

Rais Alpha Conde alisema kuwa hatua hizo zitakuchukuliwa katika maeneo ya pwani ya nchi ambapo visa vipya vya ugonjwa wa ebola vimegunduliwa.

Kati ya hatua zinazochukuliwa ni pamoja na kuyaweka kwenye karantini mahospitali na zahanati ambapo visa vipya vya ugonjwa huo vinagunduliwa pamoja na sheria mpya za kuzika maiti.

Hatua hizo zitadumu kwa muda wa siku 45.

Bwana Conde alisema kuwa licha ya visa vya ugonjwa wa ebola kupungua nchini Guinea bado kuna ugumu wa kuuangamiza kabisa ugonjwa huo.