Raia waandamana kupinga ugaidi Tunisia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Raia wa Tunisia wameandamana kupinga ugaidi nchini humo

Serikali ya Tunisia inasema kuwa askari wa usalama wamemuuwa kiongozi wa kundi la wapiganaji, lilohusika na shambulio la karibuni dhidi ya makavazi katika mji mkuu, Tunis, ambapo watu zaidi ya 20 waliuwawa.

Waziri mkuu Habib Essid alisema, raia wa Algeria, kwa jina Lokman Abu Sakhra ambaye ameelezewa kuwa gaidi hatari kabisa nchini humo aliuwawa, pamoja na wapiganaji wengine wanane, kwenye shambulio lilofanywa katika jimbo la Gafsa, magharibi kwa nchi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa kiislamu nchini Tunisia

Wapiganaji hao ni wa kundi liitwalo Ibn Nafaa Brigade.

Maelfu ya watu wameshiriki kwenye mha-dhara wa mshikamano, kupinga ugaidi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi wa Tunisia wakipiga doaria

Watu maarufu walishiriki kwenye mhadhara huo, pamoja na wageni mashuhuri, akiwemo Rais Fran├žois Hollande wa Ufaransa, Waziri mkuu wa Itali, Matteo Renzi, na kiongozi wa Wa Palestina, Mahmoud Abbas.