Saudia yawashambulia Wahouthi Yemen

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ndege za kijeshi za Saudi Arabia zimeshambulia maeneo ya WaHouthi

Ndege za jeshi la Saudi Arabia zimeshambulia maeneo kadha nchini Yemen kwa usiku wa nne katika kampeni yao dhidi ya waasi wa Houthi ambao sasa wanathibiti maeneo makubwa ya nchi hiyo.

Mfalme Salman wa Saudi Arabia mapema aliuambia mkutano wa nchi za kiarabu kuwa mashambulizi hayo yataendelea hadi kile alichokitaja kuwa mapinduzi ya waasi wa Houthi yatakapositishwa.

Kwenye mji wa kusihi wa Aden wafuasi wa rais Abdrabbu Mansour Hadi wameteka mji huo tena kutoka kwa waasi wa Houthi ambao wanaungwa mkono na Iran.

Mji wa Aden ndiyo ngome ya kisiasa ya bwana Hadi na umekuwa ukilengwa zadi na waasi wa Houthi.