DRC :Mafuriko yaleta hasara kubwa Kivu

Haki miliki ya picha kivu
Image caption DRC :Mafuriko yaleta hasara kubwa Kivu

Familia nyingi zimesalia bila makaazi baada ya mafuriko kubomoa nyumba 100 katika tarafa ya Fizi katika mji wa baraka na swima, Kivu kusini ,mashariki mwa DR Congo.

Maafa hayo yanatokana namvua kali inayo nyesha maeneo hayo.

Mifugo na mimea pia hazikusazwa, mashamba mengi nayo yameharibiwa.

Mwandishi wa BBC mashariki mwa Kongo Byobe Malenga ametuandalia taarifa ifuatayo.

Nizaidi ya siku tatu mfululizo toka nvua inayoambatana na upepo mkali pamoja na radi , inanyesha hapa mashariki mwa kongo.

Katika mji wa baraka mvua iliharibu vitu kadhaa katika mji wa baraka ambapo zaidi ya nyumba kumi na tano zimearibiwa huku mto mtambala eno la Katanga ukiaribu zaidi ya hekari mia moja za mashamba kuaribiwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mvua hiyo imehribu marabara mengi na kuathiri kwa kiwango kikubwa usafiri .

Mvua hiyo imehribu marabara mengi na kuathiri kwa kiwango kikubwa usafiri .

taarifa zinasema kuwa baadhi ya shule na makanisa pia yameharibiwa na mvua hiyo kubwa.

Baadhi ya raia wa hapa nchini wanailaumu idara ya utabiri wa hali ya hewa kwa kutotoa taarifa mapema.

Wataalamu wa mazingira wanasema huenda mvua ikanyesha kwa uwingi siku za usoni kutokana na badiliko la hali ya anga huku wakiomba itahadhari.

Katika kijiji cha Swima,mvua kali ilionyesha jana ilisababisha mto Ngovi kujaa na kuvunja kingo zake kumwaga maji yake katika eneo lililokaliwa na watu.

Nyumba nyingi zilibomolewa na kuwaacha wakaazi nje bila makao.