Kampeini za uchaguzi zaanza Uingereza

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Kampeini za uchaguzi zaanza Uingereza

Kampeni za uchaguzi mkuu nchini Uingereza zimeanza rasmi katika kinyanganyiro ambacho kinaonekana kutotabirika kabisa.

Bunge lilivunjwa muda mfupi baada ya usiku wa manane na kumaliza miaka mitano ya serikali ya umoja kati ya chama cha conservative na vyama vidogo vya democrats.

Malkia atakafanya mkutano mfupi na waziri mkuu David Cameroon kabla hajaanza shughuli zake za kisiasa.

Bwana Cameron ameahidi kuandaa kura ya maoni kuhusu uanachama wa uingereza kwenye muungano wa ulaya ikiwa atachaguliwa tena mwezi mei.

Lakini chama cha upinzani cha labour kinasema kuwa hatua hiyo ni hatari kwa makampuni ya uingereza.