Viongozi 175 waliotuhumiwa kwa ufisadi watajwa

Image caption Majina ya maafisa wakuu wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi yamewasilishwa katika mabunge Kenya chini

Orodha ya majina ya maafisa wakuu wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi imewasilishwa katika mabunge mawili

nchini Kenya huku kukiwa na mjadala mkali kuhusu jinsi orodha hiyo ilivyowasilishwa bungeni.

Kikao cha bunge la senate lilisitishwa kwa muda kuruhusu wabunge kusoma ripoti hiyo.

Katika bunge la taifa wabunge nao walitaka kuzima mjadala kuhusiana na ripoti hiyo iliyowasilisha na raia kwa misingi ya kukiuka sheria.

Robert Kiptoo ana maelezo zaidi kutoka Nairobi.

Orodha hiyo ina majina 175 ya maafisa wakuu serikalini wakiwemo mawaziri, makatibu wa wizara na maafisa wengine wa taasisi za umma na hata za kibinfasi.

Image caption Maafisa hao wa serikali sasa wameshurutishwa kungatuka madarakani

Maafisa hao wa serikali sasa wameshurutishwa kungatuka madarakani kwa muda wa siku sitini ili kuruhusu uchunguzi wa kina.

Orodha hiyo ambayo wakenya wakisubiri kwa kwa hamu na ghamu hatimaye ilijadiliwa katika mabunge yote licha ya upinzani kutoka kwa wabunge kadhaa.

Mjadala mkali uliibuka katika mabunge hayo hadi spika wa bunge la senate kusitisha kikao kwa muda kuruhusu masenate kusoma ripoti hiyo ya rais.

Hata hivyo mjadala ulipoanza wabunge wengi wanaoegemea upande wa serikali waliunga mkono wakisema vita dhidi ya ufisadi ni sharti viimarishwe.

wabunge wa upinzani nao wakijaribu kupinga mjadala huo, wakidai kuwa sheria haikufuatwa na rais alipowasilisha ripoti hiyo.

Image caption Wabunge wa upinzani wanajaribu kupinga mjadala huo

Aidha wamesema kuwa ripotio haina sahihi kama inavyohitajika.

Mpinzani mkuu wa rais Kenyatta na kiongozi wa upinzai, Raila Odinga, akiongea baada ya kuwasili nchini kenya kutoka uchina siku ya jumapili,

alisema hatua hiyo ya rais ni sawa na ulaghahi dhidi ya wakenya.

Amesema kutoka na jinsi mfumo wa mahakama upo, ni vigumu sana kwa uchunguzi dhidi ya maafisa 175 kukamilishwa kwa siku sitini ikizingatiwa

kuwa kuna baadhi ya kesi za ufisadi ambazo zimesalia mahakamani kwa zaidi ya miaka kumi.

Mjadala kuhusu ripoti hiyo ya rais inarajiwa kuendelea kwa muda wa siku tatu zijazo huku wale waliotajwa wakihitajika kungatuka madarakani hadi uchunguzi utakapokamilika.