Kane kuanza mechi ya kirafiki

Haki miliki ya picha z
Image caption Harry kane wa Tottenham

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane anatarajiwa kuanza katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa leo katika dimba la Juventus Stadium mnamo saa tano kasorobo kwa saa za Afrika Mashariki huko nchini Italy.

Mchezaji huyo kinda ambaye amekwisha tikisa nyavu mara 29 katika msimu huu akiwa na klabu yake ya Spurs, alitumia sekunde 79 tu kufunga goli baada ya kuingia akitokea benchi kuziba pengo la nahodha wake Wayne Rooney katika mchezo wa kufuzu dhidi ya Luthuania siku ya Ijumaa ambapo England ilishinda kwa jumla ya mabao 4-0. ‘’Harry anastahili kupata nafasi’’ alisema kocha wa England Roy Hodgson. ‘’ Hii ni nafasi kwa baadhi ya wachezaji kuonesha kuwa wanaubora’’ aliongeza kocha huyo.

Mpaka sasa mchezaji huyo amekwisha funga mabao 8 katika michezo 10 aliyoichezea timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 21.

Wakati hayo yakijiri Wayne Rooney amebakiza mabao mawili tu ili kufikia rekodi ya mfungaji wa wakati wote wa timu ya taifa England Sir Bobby Charlton ambaye aliweka kimiani mabao 49 katika kipindi chake cha uchezaji.