Watu kumi na tano wamekufa katika kijiji cha Kimino huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Huwezi kusikiliza tena

Mafuriko yaua watu 15 DRC

Watu kumi na tano wamekufa katika kijiji cha Kimino huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutokana na nvua kubwa inayoendelea kunyesha katika jimbo la Kivu Kusini Mashariki mwa nchi hiyo.

Mvua hizo zimesababisha uharibufu wa mkubwa wa nyumba na kuzifanya familia nyingi kubaki bila makazi, mifugo kufa na mashamba kuharibiwa vibaya.

Mwandishi wa BBC Mashariki mwa Congo BYOBE MALENGA ametutumia taarifa ifuatayo.