Iran:Mazungumzo yatazaa matunda?

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mazungumzo yanarejelewa tena hii leo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran kwenye mji wa Lausanne

Mazungumzo yanarejelewa tena hii leo kuhusu mpango wa nuklia wa Iran kwenye mji wa Lausanne nchini Uswisi zikiwa zimesalia saa chache kabla ya kumalizika kwa muda wa kuafikiwa makubaliano.

Mataifa sita yenye nguvu zaidi duniani yanakaribia kuafikia makubaliano na Iran. Hatua zimepigwa kuhusu njia za kuzuia na kufuatilia shughuli za kinuklia za Iran.

Mwandishi wa BBC mjini Lausanne anasema kuwa tofauti kubwa bado zimesalia kwenye masuala kadha ikiwemo kuhusu ni njia ipi ya haraka vikwazo dhidi ya Iran vitaondolewa.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Iran inasema mpango wake wa Nyuklia ni wa kuzalisha umeme

Waziri wa masuala ya nje wa Marekani John Kerry amesema kuwa kuna mataumaini ya kufanikisha mazungumzo hayo ila akaongeza kuwa kuna maswala ambayo bado hayajatatuliwa.

Iran inashikilia kukutu kuwa mradi wake wa Nyuklia ni wa kuzalisha umeme lakini mataifa ya Magharibi yanapinga yakihofia kuwa huenda Iran inapanga kutengeza silaha zenye nguvu za kitonaradi.

Mataifa hayo ya magharibi yanalenga kudumaza uwezo wa Iran wa kutengeza Silaha zenye nguvu za kitonaradi kwa zaidi ya mwaka mmoja ili wawaondolee vikwazo vya kiuchumi.

Image caption ''Tofauti kubwa bado zimesalia kwenye masuala kadha ikiwemo kuhusu ni njia ipi ya haraka vikwazo dhidi ya Iran vitaondolewa '' asema Kerry

Mawaziri wa maswala ya kigeni wa mataifa matano yenye nguvu zaidi duniani yaani P5+1 -

Marekani, Uingereza ,Ufaransa , Uchina, Urusi na Ujerumani na waziri wa Iran Mohammad Javad Zarif wanaendelea na mkutano huu huku makataa waliojiwekea wenyewe ikikaribia kukamilika.