Aliye waua Waingereza wawili kunyongwa

Haki miliki ya picha
Image caption Kitanzi cha kunyongea watu

Mahakama ya Malaysia imemkuta na hatia ya mauaji mtu mmoja kwa tuhuma za mauaji ya wanafunzi wawili wa udaktari kutoka nchini Uingereza.Mauaji hayo yanadaiwa kufanyika August mwakajana katika kisiwa cha Borneo.

Jaji wa mahakama hiyo amesema mahakama imeidhishwa na ushahidi dhidi ya mshitakiwa na kuona anastahili adhabu. Hukumu hiyo inayomkabili Zulkipli Abdullah anadaiwa kuwaua Neil Dalton na Aidan Brunger.

Kwa mjibu wa hukumu hiyo ya mauaji, Abbdullah atanyongwa hadi kufa.