Murray atinga robo fainali Miami Open

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Andy Murray mchezaji wa tenis wa Uingereza

Mchezaji tenis mashuhuri duniani, Andy Murray amekuwa Mwingereza wa kwanza kuweka historia ya kushinda mara 500 katika mchezo wa tenis baada ya kumwadhibu Kevin Anderson kutoka Afrika Kusini.

Murray alishinda kwa seti 6-4 3-6 6-3 na kuwa mchezaji wa 46 kushinda mara 500 tangu kuanzishwa kwa mashindano ya wazi.

Kwa ushindi huo Murray amefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali kwenye mashindano ya Miami Open.

Katika orodha hiyo ya wachezaji 46, tisa tu ndio bado wanaendelea kucheza mchezo huo.