Harakati za kuupinga ugaidi mitandaoni

Image caption Kijana Shafiq ambaye amejiunga katika harakati hizo.

Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani umebakisha miezi miwili kuwadia.Baadhi ya waislamu duniani wameamua kuanzisha mshikamano katika mitandao ya kijamii na wenzao wakristo katika mfungo wa Kwaresma ili kuonesha mshikamano na umoja miongoni mwao.

wazo hili limepata kasi baada ya ongezeko kubwa la matukio ya kigaidi kuongezeka duniani na hivyo baadhi ya waislamu waliamua kufunga kipindi hiki cha kwaresima mpaka maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka .

Harakati zimeendelea kwenye mitandao ya kijamii kwa kusambaza picha zenye ujumbe wa upendo,swala na Eid wakiwa na lengo la kuunganisha waislamu na kubadili fikra za madhehebu mengine kuhusu imani yao ya Uislamu.

Muasisi wa wazo hili la upendo, sala/swala na Eid ni Bassel Riche yeye anasema kwamba kampeni hii imekuja wakati muafaka ambapo inabidi tuuaambie ukweli ulimwengu na hivi vikundi vya kigaidi bila kuwaogopa,inabidi wafahamu sisi tunapinga kwa asilimia mia moja jinsi wanavyotumia imani yetu kufanya maovu.

Dhumuni la kufunga wakati wa kwaresima halina utofauti na funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, hivyo duniani kote wakristo kwa waislamu tunapaswa kupinga ugaidi.