Sterling asema mataji kwanza ndipo mali

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Raheem Sterling mchezaji wa Liverpool ya Uingereza

Mwanasoka wa Liverpool Raheem Sterling kuiambia BBC kwamba yeye si mpenda fedha baada ya kuthibitisha mshahara wake mpya wa £100,000 kwa wiki.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 20 ameongeza kuwa hatojadili mkataba wake mpya na klabu yake hiyo mpaka msimu wa kiangazi, haijalishi ukubwa wa mkataba ambao atapewa muda huu.

'' kwa ujumla si suala la fedha'' alisema. ''Haijawahi kuwa kuhusu fedha, nazungumzia suala la kushinda mataji katika kipindi changu chote cha uchezaji'' aliongeza kusema Sterling.

Mchezaji huyo hakusita pia kuonyesha kupuuzia suala la kuwa na nyumba za kifahari au magari mengi. Jambo la msingi kwake ni kuwa bora zaidi uwanjani.