Mtoto mpya amtesa Kim Kardashian

Image caption Kim akimpa taarifa mumewe Kanye West juu ya tatizo linalomkabili.

Mwanamama nguli na nyota wa kipindi cha runinga cha The Keeping Up with the Kardashians,Kim West ambaye ana mtoto mwenye umri wa miezi 21 North West aliyezaa na mumewe Kanye West,imeelezwa na mumewe huyo Kanye ,mkewe hataki chochote katika ulimwengu huu zaidi ya kupata mtoto mwingine ,lakini madaktari wamemuonya anaweza kukabiliwa na hatari kiafya.

Katika kipande cha kipindi kinachofuata cha kipindi cha mwanamama huyo ambacho kitarushwa katika runinga ya E’ inayojihusisha na masuala ya burudani na huenda kipande hicho kitarushwa mwishoni mwa wiki hii ,kipande hicho kinamuonesha Kim akielezea alichoambiwa na daktari wake kuwa anajaribu kumficha Kanye West anachotakiwa kwenda kufanyiwa na madaktari kuondoa kitu kilichoko kwenye kizazi chake.

Na ilipobidi kumkabili mumewe huyo, ambaye ni nguli wa muziki wa tambo,alipomwambia juu ya suala hilo tete, alikubaliana nalo na kumwambia endapo atafanikiwa kupata mtoto wa pili atakuwa wa mwisho kwasababu kondo la uzazi linakua kwenye kizazi chake.

Image caption Mke wa Kanye West

lakini baadaye mrembo huyo alionekana kukata tamaa ya kupata mtoto mwingine,na akaeleza wazi kuwa alipokuwa mjamzito wa mtoto wao wa sasa North,alikuwa akiwaambia watu wake wa karibu kwamba hakuna kiwango cha pesa duniani atakachoweza kulipwa kurejea tena katika maumivu ya uchungu wa kuzaa.

Lakini,kwasasa hakuna kitu ninachokihitaji zaidi ulimwenguni kama kuwa mjamzito tena,nina pata hasira kidogo kwamba watoto wangu wataachana miaka kadhaa.

Siku za karibuni Kim alitoa ya moyoni kwa kueleza kwamba ulikuwa ni muujiza kuipata mimba ya mtoto wake North kwasababu madaktari walisha mwambia kuwa milele hataweza kubeba ujauzito .