Nyuklia:Marekani kuafikiana na Iran

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais Obama wa Marekani

Ikulu ya white house nchini Marekani inasema kuwa rais Obama ana uhakika kuwa Marekani itaafikia makubaliano ya mwisho na Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia ifikiapo mwishoni mwa mwezi Juni.

Msemaji wa Ikulu anasema kuwa bado kuna kazi ya kufanywa kwa yale yaliyoafikiwa siku ya alhamisi licha ya wanasayansi waliyoyachunguza maafikiano hayo kusema kuwa wana uhakika kuwa yanaweza kuizuia Iran kuunda silaha za nyuklia.

Msemaji huyo wa ikulu ameongeza kuwa Marekani haitatia sahihi makubaliano ambayo yataiweka Israeli hatarini akisema kuwa Marekani inaendelea kushauriana na washirika wake katika eneo hilo.

Rais wa Iran Hassan Rouhani anasema kuwa nchi yake itaheshimu upande wake wa makubaliano hayo iwapo wengine nao watafanya hivyo.