Ugaidi:Uganda yajiweka katika tahadhari

Image caption Mkuu wa Polisi nchini Uganda Kale kayihura

Siku moja baada ya mauaji yaliyotea katika chuo cha Garissa nchini Kenya polisi katika nchi jirani ya Uganda wanasema kuwa wamepokea habari kuwa shambulizi sawa na hilo linapangwa kufanywa nchini humo.

Mkuu wa polisi nchini Uganda Kale Kayihura amesema kuwa Al shabaab linapanga kushambulia taasisi ya elimu kwenye barabara inayounganisha mji ulio mashariki wa Jinja na mji mkuu Kampala.