Kenya yaomboleza shambulizi la Garissa

Haki miliki ya picha b
Image caption kenya yaomboleza

Ikiwa siku ya kwanza ya zile tatu za maombolezi zilizotangazwa na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya imeanza kufuatia shambulizi la chuo kikuu cha Garissa,makanisa yote nchini Kenya yatajitolea kuwaombea waathiriwa wa tukio hilo wakati huu wa sikukuu ya pasaka.

Shambulizi hilo la siku ya Alhamisi liliwaacha takriban watu 150 wakiwa wameuawa.

Shirika la msalaba mwekundi nchini Kenya linasema kuwa hadi sasa maiti 54 zimetambuliwa katika chumba kimoja cha kuhifadhi maiti kwenye mji mkuu wa Kenya Nairobi.

Image caption Bendera ya kenya

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa idara za usalama zinahitaji kuongeza jitihada za kupambana na wanamgambo wa Al shabaab.

Chuo cha kutoa mafunzo ya kiislamu kinacheshimiwa zaidi nchini Misri, Al-Azhar kimelaani kile ilichokitaja kuwa shambulizi la kigaidi dhidi ya wanafunzi wasio na hatia.